Tuesday, 3 December 2019

mkakati wa kuwapokea kidato cha kwanza 2020 katika wilaya ya Kibondo


KIBONDO

Halimashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imeanza kusambaza vifaa vya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza 2020 hawakosi mahali pa kujifunzia

Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Diocres  Rutema Akizungumza wakati wa zoezi la kusambaza vifaa hivyo amesema kuwa vifaa hivyo vitakavyogharimu Zaidi ya milioni 50 ni kwa ajili ya kukamilisha maboma thelathini yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi katika shule mbali mbali

Amesema kuwa awamu ya kwanza ya ukamilishaji wa maboma hayo imeanza ambapo tayari shule 4 kati ya 10 za mwanzo zimekabidhiwa vifaa hivyo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa linapatiwa ufumbuzi

Usambazaji wa vifaa hivyo umeanzia katika shule ya sekondari maunt samba ambayo tayari wananchi wamejenga boma linalopaswa kukamilishwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza 2020 wapate mahali pa kujifunzia mkuu wa shule hiyo mwalimu Baraka msambazi amesema kuwa vifaa hivyo vilivyotolewa na serikali vitasaidia kwa kiasi kikubwa

Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Luis Bura akikabidhi vifaa vya ujenzi katika shule ya sekondari mount Samba amempongeza mkurugenzi kwa kazi nzuri na kumtaka kuendelea kutilia mkazo maagizo ya mkuu wa mkoa ya kuwasisitiza wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa maboma ili serikali iweze kukamilisha kwa kununua vifaa vya madukani. ENDS


Tuesday, 5 March 2019

Serikali yapiga marufuku kusafirisha mizigo



Serikali imepiga marufuku kusafirisha mizigo, vifurushi na bahasha kwenye magari ya abiria, mpaka kuwe na kibali maalum kutoka Mamlaka ya mawailiano nchini (TCRA)
 Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mh Mhandisi Atashasta Nditiye alipokuwa akizungumza na watumishi wa taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo ikiwemo kampuni ya simu nchini TTCL na shirika la Posta Tanzania, mjini Musoma.
Sambamba na hilo Naibu Waziri Nditiye ameitaka SUMATRA kuendesha oparesheni maalum ya kusimamia agizo hilo, na kudhibiti kabisa vitendo hivyo.
Hata hivyo amewataka watendaji wa taasisi hizo kuziendesha taasisi hizo kwa faida, ikiwa ni pamoja na kutumia vema fedha zinatolewa na serikali kuu kama ruzuku, na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji watakaobainika kwenda kinyume na maelekezo hayo.

Thursday, 28 February 2019

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATASHASTA NDITIYE ATEMBELEA TUME YA TAIIFA YA TEHAMA NA TCRA-CCC





Naibu Waziri, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya TEHAMA katika ziara hiyo

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya TEHAMA, Mhandisi Samson Mwela akitoa maelezo kwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).