KIBONDO
Halimashauri
ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imeanza kusambaza vifaa vya ujenzi wa vyumba
vya madarasa katika shule za sekondari ikiwa ni mkakati wake wa kuhakikisha
wanafunzi wa kidato cha kwanza 2020 hawakosi mahali pa kujifunzia
Mkurugenzi
mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Diocres Rutema Akizungumza wakati wa zoezi la
kusambaza vifaa hivyo amesema kuwa vifaa hivyo vitakavyogharimu Zaidi ya
milioni 50 ni kwa ajili ya kukamilisha maboma thelathini yaliyojengwa kwa nguvu
za wananchi katika shule mbali mbali
Amesema kuwa
awamu ya kwanza ya ukamilishaji wa maboma hayo imeanza ambapo tayari shule 4
kati ya 10 za mwanzo zimekabidhiwa vifaa hivyo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha
tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa linapatiwa ufumbuzi
Usambazaji
wa vifaa hivyo umeanzia katika shule ya sekondari maunt samba ambayo tayari
wananchi wamejenga boma linalopaswa kukamilishwa ili wanafunzi wa kidato cha
kwanza 2020 wapate mahali pa kujifunzia mkuu wa shule hiyo mwalimu Baraka
msambazi amesema kuwa vifaa hivyo vilivyotolewa na serikali vitasaidia kwa
kiasi kikubwa
Mkuu wa
wilaya ya kibondo bw Luis Bura akikabidhi vifaa vya ujenzi katika shule ya
sekondari mount Samba amempongeza mkurugenzi kwa kazi nzuri na kumtaka
kuendelea kutilia mkazo maagizo ya mkuu wa mkoa ya kuwasisitiza wananchi
kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa maboma ili serikali iweze kukamilisha kwa
kununua vifaa vya madukani. ENDS
No comments:
Post a Comment